PAKISTAN

Shambulizi la bomu lawauwa watu 18 ndani ya basi nchini Pakistan

Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga limesababisha vifo vya watu 18 nchini Pakistan wengi wao  wanawake.

Matangazo ya kibiashara

Polisi mjini Peshawar wanasema zaidi ya watu wengine 40 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo liliwalenga wafanyikazi wa serikali waliokuwa wanasafirishwa kwenda ofisini.

Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kuwakumba raia wa Pakistan katika siku za hivi karibuni,katika ngome inayoshukiwa kuwa ya wanagambo wa kigaidi wa Taliban.

Inakisiwa kuwa kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita, matukio kama haya yamesabisha vifo vya zaidi ya watu elfu 5, huku serikali ya Pakistan ikiilamu Marekani kwa kuwaua raia wasiokuwa na hatia wakati wanapotekeleza mashambulizi ya angaa kukabiliana na wanagambo wa Taliban.

Uhusiano wa Marekani na Pakistan umedorora kwa kipindi cha miezi sita iliyopita,baada ya wanajeshi wa kimataifa wa NATO kuwauwa wanajeshi 24 wa Pakistan katikia mpaka wake na Afganistan.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta imeonya Islamabad kuwa haifanyi juhudi za kutosha kulitokomeza  kundi la Taliban na badala yake inawapa hifadhi wanachama wa kundi hilo la kigaidi.