COTE D IVOIRE

Maelfu wakimbia makazi baada ya shambulizi Cote d Ivoire

Ramani ya Cote D Ivoire kama inavyoonekana pichani
Ramani ya Cote D Ivoire kama inavyoonekana pichani iaenzeninterviews.wordpress.com

Maelfu ya raia nchini Cote d Ivore wameyakimbia makazi yao wakihofia usalama wao baada ya walinda amani 7 kutoka umoja wa mataifa na raia 8 kuuawa katika mashambulizi ya ghafla jirani na mpaka wa nchi hiyo na Liberia.

Matangazo ya kibiashara

Afisa wa umoja wa mataifa UN na mashuhuda wa tukio hilo wamethibitisha kuwa kuendelea kuwepo kwa mawimbi ya mashambulizi kulisababisha Liberia kutangaza kufunga mipaka yake kwa jirani yake na kuhakikisha kufungwa huko hakudhuru shughuli za kawaida za kila siku katika eneo lile.

Waangalizi wa amani kutoka umoja wa mataifa  UN waliuawa ijumaa walipokuwa katika harakati za kuhakikisha hali ya usalama iko sawa baina ya vijiji viwili baada ya uvumi kusambaa kuwa kuna mpango wa shambulizi kutekelezwa katika jamii ile.

Msemaji wa umoja wa mataifa UN huko Cote d Ivoire Anouk Desgroseilliers amesema Kumekuwepo na mfululizo wa mashambulizi ya ghafla katika viji kadhaa jirani na mji wa kusini magharibi huko Tai.