DAMASCUS-SYRIA

Watu wazidi kupoteza maisha Syria,Urusi yataka Iran kushiriki kukomesha mauaji.

Mauaji ya raia Daraa nchini Syria
Mauaji ya raia Daraa nchini Syria AFP

Mashambulizi ya majeshi ya Syria yamesababisha takribani vifo 83 siku ya jumamosi,shirika la waangalizi haki za binadamu limethibitisha wakati Urusi ikishinikiza hoja yake ya mkutano wa kimataifa kufanyika ikiwemo Iran kushiriki kumaliza umwagaji damu nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisisitiza kuwa serikali ya mjini Moscow isingezuia matumizi ya nguvu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa UN.

Pendekezo hilo linakuja wakati ambapo machafuko ya Syria yameamsha hasira ya kimataifa dhidi ya utawala wa raisi Bashar al Assad ambao umesababisha mauaji ya watu 13,500 wengi wakiwa raia walIopoteza maisha tangu march mwaka jana.

Wanawake 9 na watoto 3 walikuwa ni miongoni mwa watu 20 waliouawa katika mashambulizi ya awali katika makazi ya jiji la Daraa mapema jumamosi,kwa mujibu wa waangalizi wa haki za binadamu.