Syria

Mkuu wa operesheni ya Umoja wa Mataifa nchini Syria asema nchi hiyo imeingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe

Mashambulizi ya ma bomu katika jiji la Haffe
Mashambulizi ya ma bomu katika jiji la Haffe

Mkuu wa operesheni ya Umoja wa Mataifa UN ya kulinda amani nchini Syria Herve Ladsous amesema kwamba, kwa hali iliopo kwa sasa nchini Syria, nchi hiyo inaelekea kwenye vita vya wenye kwa wenyewe wakati vita ikiendelea baina ya vikosi vya serikali ya rais Bashar Al Assad na waasi wa serikali, huku jeshi la nchi hiyo liliendelea kushambuliaa ngome ya waasi.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo amesema kwamba serikali ya Bashar Al Assad imepoteza udhibiti wa miji kadhaa kwa faida ya upinzani, ambapo sasa jeshi la Assad linajaribu kushambulia kuhakikisha miji iliotekwa na waasi inarejea mikononi mwa serikali.

Hapo jana, watu 36 waliuawa wakiwemo raia 24, ikiwa ni siku ya nne mfululizo jeshi la Syria likishambulia mji wa Haffe. Kwa mujibu wa shirika linalo tetea haki za binadamu, ma mia ya wapiganaji wa Syria wamejificha katika mji huo muhimu kufuatia mji huo kuwa karibu na Kardaha, mji aliko zaliwa rais Bashar Al Assad. Shirika hilo limesema kwa muda wa siku nane za mashambuliz watu 190 wameuawa wakiwemo raia wa kawaida 29.

Mashahidi wamesema kwamba wananchi wameuahama mji huo ambao kwa sasa umezingirwa na vifaru vya jeshi la serikali ya rais Assad.

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa UN nchini Syria umesema waangalizi wameziuliwa kuingia katika mji wa Haffe baada ya kundi kubwa la watu waliokuwa na hasira kujitokez ana kuwazuia kuendelea na shughuli zao, na hivyo kulazimika kurudi nyuma baada ya kurushiwa mawe na wananchi hao. Hata hivyo msafara huo wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa ulishambuliwa risase bila hata hivyo kudhuru chochote.

Mwanzoni mwa juma hilo Marekani ilionya kuhusu serikali ya Syria kupanga njama ya kutekeleza mauaji katika mji wa Haffe. Jana Ufaransa nayo ilijitokeza na kudaikuwa serikali ya Syria imeandaa kutekeleza mauaji na sasa wapo katika mawasiliano na viongozi wa Urusi kujaribu kutafuta suluhu ya kidiplomasia

Upande wake waziri wa syria wa mambo ya nje ameishutumu serikali ya Marekani kuyaunga mkono makundi ya waasi na kuyashinikiza kutekeleza mauaji zaidi na vitendo vya kigaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema kwamba Marekani inatiwa hofu na habari ya kutumwa kwa Helicopta za kijeshi za Rashia kuwashambulia wananchi wa Syria.

Nae waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anasubiriwa nchini Iran. Serikali ya Iran imesema ipo tayari kuunga mkono pendekezo la Urusi la kuandaa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria huku Iran ikishiriki.