Myanmar

muakilishi wa Ban ki Moon awasili nchini Myanmar

polisi wa myanmar (Reuters)
polisi wa myanmar (Reuters) Reuters

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,Vijay Nambiar, amewasili Magharibi mwa nchi ya Mnyamar eneo ambalo linakumbwa na makabiliano ya kidini.

Matangazo ya kibiashara

Nambiar yupo katika jimbo hilo la Rakhine kujaribu kusuluhisha makabiliano hayo amabyo yamesababisha kuuawa kwa zaidi ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 40 katika mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku tano zilizopita.

Hali ya hatari ilitanazgwa katika jimbo hilo baada ya kuanza kwa makabliano hayo kati ya waislamu na wabudha, baada ya mwanamke wa Kibudha kubakwa na kuuliwa, mauji yanayotuhumiwa kutekelezwa na waislamu.

Jumuiya ya kimataifa imeshtumu makabiliano hayo ya kikatiba ambayo yanarudisha nyuma juhudi za kidemokrasia na kuheshimu haki za binadamu zinapigwa katika taifa hilo.

Myanmar imekuwa chini ya vikwazo vya jamii ya kimataifa tangu miongo kadhaa, lakini baadhi ya nchi tayari zimetangaza kulegeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo, kufuatia mabadiliko ya uongozi yanayo piga hatuwa ya kuridhisha.