Myanmar

Aung San Suu Kyi na ziarani barani ulaya

A líder democrática de Myanmar, Aung San Suu Kyi, embarca no aeroporto internacional de Yangon para sua viagem à Europa nesta quarta-feira.
A líder democrática de Myanmar, Aung San Suu Kyi, embarca no aeroporto internacional de Yangon para sua viagem à Europa nesta quarta-feira. REUTERS/Minzayar

Kiongozi wa upinzani nchini Mynamar Aung San Suu Kyi ameianza ziara ya wiki mbili barani ulaya ambapo atazuru Usuisi, Norway, Uingereza ambako alikosomea, Irland na Ufaransa. Hapo jana Suu Kyi amewasili jijini Geneva ambako anatarajia kuhutubia katika kikao cha kimataifa cha shirika la ajira duniani

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Aung San Suu Kyi inajiri wakati machafuko yakiendelea kuripotiwa katika jimbo la Arakane nchini Myanmar, na ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo barani Ulaya tangu alipotumikia kifungo cha nyumbani.

Mwaka 1991 Mumewe ambae tayari ni marehemu pamoja na wanae wawili ndio ambao walipokea medani na cheti pamoja na fedha jijini Oslo wakati alipotunukiwa taji la Amani la Nobel. Hata hivyo sherehe rasmi zinazofanyika katika kutoa taji hilo hazikufanyika. Suu Kyi anatarajia kuhutubia jijini Oslo katika sherehe za kupewa taji lake la Nobel siku ya Jumamosi.

Hotuba ya Su kyi bila shaka itakuwa tofauti na ile ambayo huenda angelitowa wakati ule jeshi lilikuwa mamlakani nchini mwake likiendesha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia.

Kiongozi huyo wa upinzani ambae ni mbunge wa myanmar kwa sasa aonekana kuwa na nguvu nchini mwake na utawala uliopo unamtegemea katika kupeleka sifa za hatuwa iliopigwa nchini humo katika kudumisha demokrasia.