MALI-UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili ombi la kutuma vikosi nchini Mali

Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Umoja wa Afrika umeomba baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kuunga mkono uingiliaji kijehi katika mzozo wa Mali. Mashirika hayo yamejadili swala hilo jana Juni 13 katika kikao kilichofanyika jijini Neew York Marekani. Hata hivyo baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema mpango uliowsilishwa na Umoja wa Afrika na ECOWAS hauko wazi, hivyo kiko kingine kujadili swaal hilo kimepangwa kufanyika siku ya Ijumaa jijini New York.

Matangazo ya kibiashara

Baraqza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejiweka kando na ombi la Umoja wa Afrika kutuma vikosi nchini Mali chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa. Wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hawakuweka kando uwezekano wa uingiliaji kijeshi nchini Mali, lakini wamesema mpango uliowasilishw ana Umoja wa Afrika na ECOWAS haukuweka bayana hasa kuhusu lengo.

Mathalan baraza la usalama linataka uwepo mpango wa kisiasa baada ya uingiliaji kijeshi. Marekani yao yataka viwekwe vikwazo kwanza kabla ya kuingilia kijeshi.

Iwapo majeshi yatatumwa, itakuwa ni operesheni ya uvamizi kijeshi au ni operesheni tu ya kusaidia vikosi vya Mali katika shughuli za ulinzi? Ni askari wangapi wataotumwa nchini Mali na kwa gharama gani? Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lasubiri majibu kuhusu maswali hayo.

Swala la Mali linajadiliwa katika nchi nyingi wakati huu. Mbali na New York Marekani, Mali yajadiliwa pia nchini Alger na Ufaransa.

Waziri mkuu wa Mali Cheikh Modibo Diarra akiwa ziarani jana nchini Algeria amekutana na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo na kujadili kuhusu hali ya kaskazini mwa Mali.

Waziri Diarra anaelekea jijini Paris Ufaransa ambako Ufaransa inaunga mkono uingiliaji kijeshi nchini Mali. Cheikh Modibo Diarra atakutana pia na rais wa mpito wa Mali Diouncounda Traore anaepata matibabu jijini Paris.

Ijumaa Juni 15 macho yote yataelekezwa New York Marekani ambako swala la Mali litawekwa tena mezani.