DRCongo-icc

Kifungo cha miaka 30 jela kwa kiongozi wa zamani wa uasi katika jimbo la Ituri Thomas Lubanga

Thomas Lubanga
Thomas Lubanga

Mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC, imepanga kumuhukumu kifungo cha miaka 30 jela kiongozi wa zamani wa kundi la uasi Thomas Lubanga kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Kesi hiyo ya kiongozi wa zamani wa kundi la FPLC ni ya kwanza katika mahakama hiyo na ilizinduliwa januari 2009 na kuhitimishwa Agosti 26 mwaka 2011 ambapi Thomas Lubanga aliendelea kujitetea kuwa hana hatia.

Matangazo ya kibiashara

Miaka 30 jela, hiyo ndio hukumu iliotolewa kwa Thomas Lubanga, na huenda jaji wa mahakama anaweza kugeuza hukumu hiyo na kumuhukumu kifungo cha maisha jela iwapo jaji huyo atachukulia kwamba makosa aliyoyatekeleza Tjhomas Lubanga ni makubwa mno. Louis Moreno Ocampo amesema hukumu hiyo itakuwa mfano kwa wengine.

Ocampo amemtaka Thomas Lubanga kuomba radhi kutokana na makosa aliyoyatekeleza katika jimbo la Ituri. Hat hivyo tarehe rasmi ya kusomewa hukumu haikutajwa

kulingana na mashirika ya kiraia Machafuko katika jimbo la Ituri yalisabisha vifo vya watu elfu sitini mwaka 1999. Thomas Lubanga alikamatwa tangu mwaka 2006 na kupelekwa katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC ilioko the Hege nchini Uholanzi.

Mahakama hiyo ilimkuta na makosa ya uhalifu wa kivita Machi 14 kutokana na makosa yaliotekelezwa mwaka 2002 na 2003. Lubanga anatuhumiwa makosa ya kuwatumia watoto wadogo katika jeshi lake katika machafuko yaliotokea jimboni Ituri kaskazini mashariki mwa DRCongo.