Ufaransa-Italia

Rais wa Ufaransa Francois Hollande kukutana na waziri mkuu wa Italia Mario Monti

rais wa Ufaransa Francois Hollande na Mario Monti
rais wa Ufaransa Francois Hollande na Mario Monti REUTERS/Michel Euler/

Raisi wa ufaransa Francois Hollande anataraji kuanza mazungumzo na waziri mkuu wa italia Mario Monti hii leo wakati italia ikikabiliana na uvumi juu ya kusaidiwa kuokoa uchumi wake unadorora.

Matangazo ya kibiashara

ziara ya raisi Holande nchini italia inakuja kufuatia hofu iliyoibuka kwamba viongozi wa ukanda wa yuro wameshindwa kudhibiti hali ya mgogoro wa uchumi ambao umeilazimu uhispania kuomba misaada na huenda ikashuhudia ugiriki ikijiondoa katika ukanda huo mara baada ya uchaguzi mwishoni mwa juma hili.

Shinikizo kwa viongozi wa umoja wa ulaya kukubaliana na hatua dhidi ya mgogoro huo zimedhihirishwa na kujirudia huko italia.

Mkutano wa viongozi hao unakuja wakati waziri mkuu wa italia mario monti akijaribu mbinu za kupambana na hali mbaya ya uchumi na kuanzisha harakati pana za kujadili mgogoro wa uchumi na kuipa italia majukumu makubwa.

Mazungumzo ya alhamisi yanatazamiwa kujikita katika ukuaji na jinsi ya kudhibiti madeni ambavyo vitaweka msingi wa mkutano mkuu wa kilele kati ya italia,ufaransa,ujerumani na uhispania siku ya 22 june na mkutano mkuu wa viongozi wa umoja wa ulaya huko brussels wa june 28-29.