Togo

Upinzani nchini Togo watoa wito kwa wananchi kusalia nyumbani Ijumaa hii

La manifestation a été réprimée par les forces de l'ordre qui ont tiré des gaz lacrymogènes.
La manifestation a été réprimée par les forces de l'ordre qui ont tiré des gaz lacrymogènes. Facebook/ #OccupyLome/ D.R.

Polisi nchini Togo imepambana na waandamanaji katika kujaribu kuzima maandamano ya wanaharakati wa muungano wa “Tuisaidia Togo” wanaoandamana jijini Lome kwa siku ya pili mfululizo wakipinga uamuzi wa bunge kurekebisha baadhi ya vipengele vya sheria ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Polisi ililazimika kutumia bomu za kutoa machozi katika kuzima maandamano hayo, hali ilioplekea wengi kujeruhiwa. Shirika lilalo tetea haki za binadamu nchini humo limelaani matumizi hayo ya nguvu na badala yake limependekeza majadiliano.

Muungano wa Tuisaidie Togo unajumusiha vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia, ulitowa muda wa kuandamana siku tatu mfululizo kuanzia jumanne. Muungano huo unatowa wito wa kusalia nyumbani Ijumaa hii Juni 15 kupinga matumizi ya nguvu katika kuzima maandamano ya siku tatu na unaomba waachiwe huru waandamanji waliotiwa nguvuni.

Maandamano hayo yaliandaliwa kwa sehemu moja kupinga uamuzi wa bunge la nchi hiyo kupasisha sheria ya marekebisho ya baadhi ya sheria zihusuzo uchaguzi. Miongoni mwa sheria hizo ni kuongeza idadi ya wabunge kutoka 81 hadi 91 katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika Octoba ijayo.

Upinzani na mashirika ya kiraia nchini humo unaomba sheria hiyo ya marekebisho ya haerha ya uchaguzi ifutwe, na muda wa uchaguzi wa bunge usogezwe mbele ili kufaanikisha uchaguzi wa kidemokrasia ulio huru na haki. Serikali upande wake imeomba ghasia zipungue kwanza kwani hakuna mazungumzo yanayo wezekana kufanyika katika hali ya vurugu.

Msemaji wa serikali ya Togo Pascal Bodjona amesema kwamba sheria ya katiba sio bibilia ambayo huwezi kubadili chochote. Kubadili sheria ya uchaguzi amesema ni jambo la kawaida. Upinzani wao, unasema magauzi hayo yanakinufaisha pekee chama tawala.