MISRI

Matokeo ya uchaguzi wa leo,kutegua kitendawili cha nani raisi Misri.

Wapiga kura nchini Misri wakiwa katika mistari tayari kuelekea chumba cha kupigia kura
Wapiga kura nchini Misri wakiwa katika mistari tayari kuelekea chumba cha kupigia kura tbc.go.tz

Wapiga kura nchini misri wanapiga kura rasmi leo ikiwa ni ngwe ya pili ambayo huenda matokeo yake yakategua kitendawili cha nani ataibuka mshindi wa kiti cha uraisi kufuatia mchuano mkali baina ya kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood Mohamed Morsi dhidi ya waziri mkuu wa zamani Ahmed Shafiq.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo limefunguliwa rasmi saa kumina mbili alfajiri ambapo wapigakura wasiopungua milioni 50 wanatarajiwa kujitokeza kupiga kura ,huku ulinzi ukiimarishwa maeneo yote kwa wanajeshi laki moja na nusu kusambazwa maeneo yote nchini humo.

Mbio hizo za uchaguzi na wagombea wake zimeigawa misri kwa kuwepo wanaohofia kumchagua shafiq kutarejesha serikali ya imla kama ya zamani,huku wengine wakihofia kupoteza uhuru binafsi ikiwa kitachaguliwa chama cha kiislamu jambo ambalo wanaliona ni vema kuitenga dini na siasa.

Uchaguzi nchini Misri unafanyika leo ikiwa ni siku chache tangu mahakama itupilie mbali hoja za kumwondoa Ahmed Shafiq katika kinyang'anyiro cha uraisi,jambo ambalo awali lilisababisha maandamano ya raia nchini Misri.