KENYA

Miaka 20 baada ya kuanzishwa kama hatua ya dharura kambi ya wakimbizi ya daadab yawa tishio kwa usalama wa wakaazi.

wfp.org

Kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyopo Mashariki mwa Kenya iliyoanzishwa kama hatua ya dharura miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuhifadhi wakimbizi wa Somalia imefurika na kuwa kambi kubwa ulimwenguni na kuwa njiapanda kwa wataalamu na kifungo cha nje kwa wakazi wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa na wakaazi zaidi ya 465,000 mwishoni mwa Mei, hali ya afya na hali ya kijamii imetajwa kuendelea kushuka huku ukosefu wa usalama ukitajwa kuwa changamoto hali inayosababisha serikali ya Kenya kukosa uvumilivu.

Kambi hiyo ya Daadab ilianzishwa mwaka 1992 katika maeneo kame ya kaskazini mashariki mwa Kenya, karibu kilomita 100 kutoka mpaka wa Somalia, kama hatua ya dharura kwa wakati huo dhidi ya wakimbizi wa Somalia waliokuwa wakikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe kufuatia kuanguka kwa rais Mohamed Siad Barre.

Hata hivyo mambo yaliendelea kuwa mabaya nchini Somalia kutokana na kuendelea kwa machafuko ambayo yalichochewa zaidi na ukame na kusababisha janga la kibinadamu hususan mwaka uliopita baada ya maelfu ya wasomalia kupoteza maisha kutokana na njaa.