UGIRIKI

Ugiriki yapiga kura kuamua kubaki katika ukanda wa sarafu ya euro au la.

Mhubiri wa kanisa la Orthodox nchini Ugiriki akipiga kura mapema leo asubuhi.
Mhubiri wa kanisa la Orthodox nchini Ugiriki akipiga kura mapema leo asubuhi. uk.reuters.com

Ugiriki inapiga kura katika uchaguzi muhimu utakao amua iwapo nchi hiyo itaendelea kusalia katika umoja wa nchi za ukanda wa Ulaya kwa kukubali kutekeleza masharti ya mkopo kwa kubana matumizi.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kupiga kura limefunguliwa mapema nchini Ugiriki kwa ajili ya uchaguzi huo muhimu ambao utaamua kama taifa hilo litakamilisha mpango wa kubana matumizi ama litahatarisha mustakabali wake katika ukanda wa sarafu ya Euro.

Raia wapatao milioni 9.8 Wa taifa hilo wameanza kupiga kura mapema alfajiri ya leo katika kile kinachotarajiwa kuwa mashindano ya karibu kati ya chama kinachounga mkono hatua za kubana matumizi na na chama cha mlengo wa kushoto kinachopinga hatua hizo.

Shinikizo limejengeka kwa Ugiriki ambayo inajitahidi tangu wiki iliyopita kuchagua kwa makini serikali ijayo huku mwelekeo wa kufungiwa mkopo ambao utahatarisha uchumi wake ambao tayari ni dhaifu ukionekana wazi kwa sasa.