UFARANSA

Chama cha Socialist kinachoongozwa na Rais Francois Hollande chaelezwa kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa Ubunge

Rais wa Ufaransa, François Hollande ambaye chama chake cha Socialist kimeelzwa kunyakua viti vingi vya Ubunge
Rais wa Ufaransa, François Hollande ambaye chama chake cha Socialist kimeelzwa kunyakua viti vingi vya Ubunge Reuters/Max Rossi

Chama cha Socialist nchini Ufaransa kinachoongozwa na rais Francois Hollande kimeelezwa kupata kura za kutosha kukiwezesha kuongoza bunge la nchi hiyo kwenye uchaguzi ambao ulifanyika miwshoni mwa juma. 

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ambao ulilazimika kuingia kwenye duru la pili baada ya uchaguzi wa awali chama hicho kushindwa kupata idadi ya kura ambazo zingekiwezesha kutawala bunge la nchi hiyo, sasa inamaana kuwa chama cha Socialist kitakuwa na wabunge wengi.

Wakati matokeo rasmi yakiwa bado hayajatangazwa na wizara ya mambo ya ndani yenye dhamana ya kufanya matokeo ya awali yanaonyesha chama hicho kupata ushindi wa viti 313 au 315 kati ya viti 577 vya bunge la nchi hiyo.

Endapo matokeo hayo yatabakia kama yalivyo basi chama cha Socialist kitakuwa na nguvu kubwa kwenye bunge lijalo ambapo sasa itakiwezesha chama hicho kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya kodi ambayo yalikuwa hatihati kupitishwa endapo chama hicho kisingepata ushindi wa jumla.

Hata hivyo uchaguzi huo wa raundi ya pili umeelezwa kuwa na idadi ndogo ya watu waliojitokeza kwenye kupiga kura ambapo idadi ya watu imeelezwa kuwa ni asilimia 55.9 ukilinganisha na ule wa duru ya kwanza.