MOSCOW-URUSI

Mazungumzo kuhusu mpango wa Nyuklia wa nchi ya Iran yameanza mjini Moscow, Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov ambaye nchi yake ni mwenyeji wa mazungumzo ya Iran
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov ambaye nchi yake ni mwenyeji wa mazungumzo ya Iran REUTERS/Maxim Shemetov

Mazungumzo ya mpango wa Nyklia kwa nchi ya Iran hatimaye yameanza rasmi mjini Moscow Urusi ambapo wajumbe wameanza kujadili mapendekezo ya awali yaliyowasilishwa kwa Ira utekelezaji wake. 

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ya siku mbili yanatarajiwa kutoka na maazimio ambayo yatanufaisha pande zote mbili ambazo zinashiriki mazungumzo hayo ambayo hata hivyo bado kuna wasiwasi wa kufikiwa makubaliano.

Mazungumzo haya ya Moscow yanafanyika kufuatia kushinidika kwa mazungumzo ya awali yaliyofanyika mjini Baghdad Iraq na mjini Istanbul Uturuki ambapo wajumbe hawakuweza kufikia muafaka kuhusu suala la Nyuklia ya Iran.

Mazungumzo hayo ambayo yanahusisha nchi Sita duniani ambazo ni watumiaji wa Nyuklia yanatarajia kugubikwa na mijadala mbalimbali ikiwemo hatua ya Iran kutishia kujitoa kwenye mazungumzo hayo iwapo hoja zake hazitasikilizwa.

Mazungumzo hayo yanakuja kufuatia waangalizi wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Nyuklia kutoa ripoti ambayo inaonyesha nchi ya Iran kuendelea na mpango wake wa kurutubisha Nyuklia kwa kutengeneza silaha za maangamizi ambazo zinahatarisha usalama wa dunia.

Wachamabuzi wa mambo wanaona kuwa mazungumzo hayo yanaweza kugonga mwamba iwapo wajumbe wa mkutano wataendelea na mapendekezo ya awali ya Istanbul na Baghdad ambayo nchi ya Iran ilisema haitatekeleza.

Serikali ya Iran tayari imeweka msimamo wake kuhusu mazungumzo hayo na kudai kuwa iwapo kutakuwa na shinikizo lolote kuhusu mpango wake wa Nyuklia haitasita kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa ana imani kuwa mazungumzo ya safari hii yatazaa matunda.