MEXICO

Nchi za G20 wataka mataifa ya Ulaya kukabiliana na mdororo wa kiuchumi kwenye mataifa yao

Picha za sanamu zikiwaonesha viongozi ambao wanashiriki mkutano wa G20 nchini Mexico
Picha za sanamu zikiwaonesha viongozi ambao wanashiriki mkutano wa G20 nchini Mexico

Viongozi wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani wanaohudhuria mkutano wa G20 nchini Mexico wametoa wito kwa nchi za Ulaya kuhakikisha zinakabiliana na mdororo wa kiuchumi ambao unaathiri uchumi wa mataifa mengi kwa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya EU Manuel Barroso akizungumza kwenye mkutano huo amesema kuwa hali ya mtikisiko wa uchumi kwenye mataifa ya Ulaya imeendelea kuwa mbaya na mataifa mengi yanahitaji msaada wa haraka wa kifedha.

Mkutano huo ambao unawajumuisha viongozi toka nchi za India, China, Marekani, Afrika Kusini, Urusi na Brazili umelenga kujadili masuala ya mtikisiko wa uchumi kwenye bara la Ulaya na kuangalia uwezekano wa kuongeza fungu la fedha kwaajili ya ukopeshaji.

Awali shirika la fedha duniani IMF liliziomba nchi wanachama za G20 kuongeza kiasi kikingine cha fedha lwenye taasisi hiyo ili kuiwezesha kutoa mikopo kwa mataifa ambayo yameingia kwenye mtikisiko wa uchumi na kuhitaji msaada wa haraka.

Mbali na mjadala kuhusu mdororo wa kiuchumi barani Ulaya, nchi wanachama pia zimekuwa na mzungumzo kuhusu hali ya mambo nchini Syria pamoja na mazungumzo kuhusu mpango wa Iran kuendelea kurutubisha Nyuklia.