ATHENS-UGIRIKI

Vyama vitatu nchini Ugiriki vinakutana kukamilisha uundwaji wa Serikali ya muungano

Antonis Samaras wa kwanza mbele akifuatiwa na Evangelos Venizelos, viongozi hawa wanajaribu kuunda Serikali ya Umoja
Antonis Samaras wa kwanza mbele akifuatiwa na Evangelos Venizelos, viongozi hawa wanajaribu kuunda Serikali ya Umoja Reuters

Viongozi wa vyama vitatu nchini Ugiriki wanaendelea na mazungumzo yao hii leo ikiwa ni siku yao ya mwisho kuhakikisha kuwa wanaunda serikali ya muungano baada ya kushindikana kwa siku ya pili hapo jana.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha New Democracy ambacho ndicho kiliibuka mshindi kwenye uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili, kimeendelea kuvishawishi chama cha Pasok na Democratic kukubali kuingia kwenye Serikali ya muungano.

Kiongozi wa chama hicho Antonis Samaras ndiye atakeyeongoza Serikali itakayoundwa ingawa mpaka sasa anakabiliwa na wakati mguu wa kuhakikisha hii leo Serikali inapatikana.

Kwa upande wake kiongozi wa chama cha Pasok, Evangelos Venizelos amesema kuwa ana imani kubwa ya kwamba Serikali mpya itaundwa hii leo hata kabla ya kuingoa usiku kwakuwa asilimia kubwa ya mambo wamekwishayajadili.

Shinikizo zaidi limeendelea kuwekwa kwa nchi ya Ugiriki hasa kwa wanasiasa kuhakikisha kuwa wanapata Serikali ambayo itahakikisha inakabiliana na mdororo wa kiuchumi ambao umeendelea kuikumba nchi hiyo.

Tayari chama cha Syriza kinachoongozwa na Alexis Tsipras kimetangaza kutojumuika kwenye serikali ya muungano itakayoundwa.