JAKARTA-INDONESIA

Mahakama kuu nchini Indonesia imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela mtuhumiwa wa mashambulizi ya mjini Bali mwaka 2002, Umar Patek

Umar Patek mtuhumiwa wa mashambulizi ya Bali ya mwaka 2002
Umar Patek mtuhumiwa wa mashambulizi ya Bali ya mwaka 2002 Reuters

Hatimaye mahakama kuu nchini Indonesia imetoa hukumu dhidi ya mtuhumiwa wa mashambulizi ya mjini Bali ya mwaka 2002 Umar Patek na kumuhuku kwenda jela miaka 20.

Matangazo ya kibiashara

Jaji aliyekuwa anasoma hukumu hiyo amesema kuwa mahakama imejiridhisha bila shaka kuwa mtuhumiwa huyo alishiriki kikamilifu kwenye mpango wa kutekeleza mashambulizi hayo yaliyoua watu zaidi ya 200.

Umar Patek amekutwa na hatua ya makosa yote ambayo alikuwa akituhumiwa nayo ikiwemo kupanga njama za ugaidi, kushirikiana na vikundi vya kigaidi, utengenezaji wa bomu na kutekeleza ugaidi kwenye mji wa Bali.

Baadhi ya wananchi wamepongeza hukumu hiyo wakiwemo ndugu wa watu waliopoteza maisha kwenye mashambulizi hayo lakini pia wapo ambao wanaona hukumu aliyopewa Patek ni ndogo kulingana na makosa aliyotenda.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama kuu kumuhukumu kifungo cha maisha jela mtuhumiwa huyo ambaye walisema licha ya kukiri kuhusika kuchanganya kemikali zilizotumika kwenye shambulio hilo bado alistahili kwenda jela muda mrefu zaidi.

Patek mwenye wakati wa kesi yake alikiri kushiriki kuchanganya kemikali ambayo ilitumika kwenye mashambulizi lakini akakataa kushiriki moja kwa moja kutekeleza shambulio lile.

Hukumu hiyo huenda ikawa ni hukumu ya kwanza na kubwa kuwahi kutolewa na mahakama kuu kwa mtuhumiwa wa ugaidi.