Burundi-sheria

Mwandishi wa habari wa Burundi Hassan Ruvakuki ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Mwandishi wa habari wa Burundi, Hassan Ruvakuki
Mwandishi wa habari wa Burundi, Hassan Ruvakuki Reuters

Mahakama kuu Mkoani Cankuzo kaskazini mwa Burundi imemuhukumu kifungo cha maisha jela muandishi wa habari wa radio Bonesha FM na Ripota wa idhaa ya kiswahili ya RFI-FRANCE 24 Hassan Ruvakuki na kundi la watu wengine wanaoelezwa kuwa magaidi, hukumu iliokosolewa na waangalizi wa maswala ya vyombo vya habari. Kesi hiyo imeelezwa kuwa ya kugofya na yenye kukandamiza vyombo vya habari nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Radio France Internationale na France 24 imesema inasikitishwa na maamuzi hayo ya mahakama kumchukulia Hassan Ruvakuki hatuwa nzito kama hiyo wakati ambapo alikuwa katika shughuli zake za kila siku.

Hukumu hiyo imetolewa jana jioni na kuleta maskitiko makubwa miongozi mwa wanahabari zaidi ya ishirini waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha Habari jijini Bujumbura.

Hassan ruvakuki amehukumiwa na watu wengine kumi na watatu ambao nao pia walihukumiwa kifungo cha maisha jela, huku wengine tisa wakihukumiwa kifungo cha miaka kumi na mitano jela kwa kosa hilo hilo.

Hassana Ruvakuki alikamatwa tangu Novemba 2011 jijini Bujumbura kwa tuhuma za kushiriki katika ghafla ya uundwaji wa kundi jipya la uasi nchini Burundi lenye makao yake nchini Tanzania, kundi ambalo baadae liliendesha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali ya burundi katika Mkoa wa Cankuzo mpakani na Tanzania.

Kesi hiyo ya Ruvakuki ilijawa tangu mwanzo na dosari na uvunjaji sheria uliosababisha mawakili wa Ruvakuki na wengine kujiondowa katika kesi hiyo wakipinga uvunjaji wa sheria.

Mkurugenzi mkuu wa radio Bonesha FM aliyokuwa akifanyia kazi Hassan Ruvakuki, amesema hukumu hiyo ni aibu kubwa kwa vyombo vya sheria nchini Burundi kumuhukumu muandishi wa habari ambae alikuwa katika shughuli.