AMMAN-JORDAN

Rubani wa ndege ya kivita aina ya Mig 21 ya Syria atua nchini Jordan na kuomba hifadhi ya kisiasa

Moshi ukifuka toka kwenye moja ya majengo kwenye mji wa Homs baada ya kushambuliwa
Moshi ukifuka toka kwenye moja ya majengo kwenye mji wa Homs baada ya kushambuliwa REUTERS/Shaam News Network

Rubani mmoja wa ndege ya kivta ya Syria ametua kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi nchini Jordan na kuomba mamlaka nchini humo kumpatia hifadhi ya kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mawasiliano wa Jordan, Samih al-Maaytah maethibitisha kutua kwa ndege hiyo pamoja na rubani yake mwenye cheo cha ukanali na kwamba wameshafanya nae mahojiano na ameomba kutorejeshwa nchini mwake.

Waziri huoy ameongeza kuwa mara baada ya mahojiano ya muda mrefu na rubani huyo aliyekuwa akiendesha ndege ya kivita aina ya Mig 21 aliomba kutua kwenye uwanja huo wa jeshi la Jordan akidai kuwa anatokea nchini Syria.

Awali televisheni ya taifa ya syria ilitangaza kupotea kwa ndege ya kivita aina ya Mig 21 ambayo ilipotea wakati wa mazoezi ingawa hawajathibitisha kama rubani aliyekuwa akiendesha ndege hiyo ndie mwenye ndege iliyopotea.

Ndege hiyo imeelezwa kuwa miongoni mwa ndege ambazo zimekuwa zikitumika na majeshi ya Syria kufanya mashambulizi ya anga kwenye mji wa Homs.

Wakati huohuo wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu duniani wameanza harakati za kuelekea kwenye mji wa Homs baada ya kukiri kuruhusiwa na mamlaka ya Syria kuingia kwenye mji huo kutoa msaada.