CAIRO-MISRI

Wananchi wa Misri waapa kuendelea na maandamano kushinikiza matokeo ya urais kutangazwa

Wananchi wa Misri wanaoendelea kuandamana kwenye uwanja wa Tahrir mjini Cairo
Wananchi wa Misri wanaoendelea kuandamana kwenye uwanja wa Tahrir mjini Cairo Reuters/Asmaa Waguih

Maelfu ya wananchi nchini Misri wameendelea kukusanyika kwenye uwanja wa Tahrir mjini Cairo kushinikiza tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo kutangaza matokeo ya urais.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano tume ya taifa ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo ya urais nchini humo lakini baadae ilisitisha kufanya hivyo kwa kile ilichoeleza kuwa inashughulikia kwanza madai ambayo yamewasilishwa na wagombea wote wawili.

Awali mgombea wa chama cha Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi alidai kuwa ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 52, hatua ambayo hata hivyo imepingwa na aliyewakuwa waziri mkuu kwenye serikali iliyoangushwa Ahmed Shafiq anaye nae anaai kushinda kiti hicho.

Hapo jana kwa mara ya kwanza Shafiq alijitokeza mbele ya waandishi wa habari kueleza kile ambacho upande wa upinzani umedai kushinda uchaguzi huo, na kuwaita wapinzani ni wanafiki kwakuwa hakuna ambaye anajua matokeo rasmi zaidi ya tume ya uchaguzi nchini.

Shafiq ameenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa ni wazi yeye ndiye msihindi kwenye kinyang'anyiro hicho na kwamba atakuwa tayari kufanya kazi na Musri pale matokeo yatakapotangazwa.

Hii leo mkusanyiko wa watu unatarajiwa kuongezeka maradufu kwenye uwanja wa Tahrir mara baada ya sala ya Ijumaa ambapo wananchi wameapa kufanya maandamano makubwa kupinga utawala wa kijeshi nchini humo.