MISRI

Homa ya matokeo ya uchaguzi Misri kushuka leo baada ya tume kutangaza mshindi

Wanachama wa Muslim Brotherhood nchini Misri wakiandamana kuelekea viwanja vya Tahrir walikoapa kuyasubiri matokeo ya uchaguzi yatangazwe.
Wanachama wa Muslim Brotherhood nchini Misri wakiandamana kuelekea viwanja vya Tahrir walikoapa kuyasubiri matokeo ya uchaguzi yatangazwe.

Hatimaye matokeo ya uchaguzi wa raisi nchini Misri kujulikana leo baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kuyabainisha wakati wowote siku ya jumapili,huku kukiwa na kimuhemuhe cha kujulikana kwa mshindi baada ya mchuano mkali baina ya Mohammed Morsi na waziri mkuu wa zamani katika uongozi uliopita Ahmed Shafiq.

Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi ilijitokeza nchini humo huku mamia ya wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood wakiapa kuendelea kukesha kwenye viwanja vya Tahrir mpaka matokeo yatakapotangazwa.

Morsi na Shafiq kila mmoja kwa upande wake wamekuwa wakidai kuwa warithi wa aliyekuwa raisi wa nchi hiyo Hosni Mubaraq,hali iiyoleta hofu miongoni mwa kambi hizo pinzani na kusababisha tume kuahirisha kutangaza matokeo hapo awali.