JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Congo yakosoa kukamatwa kwa wanachama wa upinzani.

Mwenyekiti wa jumuiya ya mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini DRC Jean Claude Katende.
Mwenyekiti wa jumuiya ya mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini DRC Jean Claude Katende. kiswahili.rfi.fr

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yamekosoa vikali hatua ya kuendelea kukamatwa kwa wanachama wa chama cha upinzani cha UDPS kinachoongozwa na Ettiene Tshisekedi wa Mulumba.

Matangazo ya kibiashara

Serikali nchini DRC imekuwa ikifanya misako ya mara kwa mara na kuwatia nguvuni wanachama wa UDPS kinacho onekana kuwa na nguvu zaidi nchini humo kutokana na kiongozi wake Ettiene Tshisekedi kukabiliana na rais Rais Joseph Kabila Kabange kwenye uchaguzi.

Mwenyekeiti wa jumuiya ya mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini DRC asadho, Jean Claude Katende amesema kuwa sheria haijatumika katika kuwakamata wafuasi hao wa chama cha UDPS.