MISRI

Morsi aapa kuiongoza Misri kwa kufuata misingi ya sheria.

Rais mpya wa Misri Mohamed Morsi
Rais mpya wa Misri Mohamed Morsi REUTERS/Ahmed Jadallah

Rais mpya wa Misri Mohamed Morsi kutoka chama cha Muslim Brotherhood ameapa kuongoza nchi hiyo kwa kufuata misingi ya sheria na hatothubutu kuwatenga raia kutokana na kabila zao ama ama imani za kidini walizonazo.

Matangazo ya kibiashara

Morsi ametoa kauli hiyo wakati akilihutubia taifa hilo kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo kufuatia ushindi aloupata wa asilimia 51.7 katika duru la pili la uchaguzi wa urais.

Aidha ametoa wito kwa raia wote wa Misri kuimarisha umoja wa taifa hilo na kuongeza kuwa umoja wa kitaifa ndio ngao pekee ya kuisaidia nchi hiyo kupita katika nyakati ngumu za kujenga taifa.

Morsi amefanikiwa kumuangusha mpinzani wake ambaye alikuwa waziri mkuu wa zamani katika utawala wa Hosni Mubarak, Ahmed Shafiq.