MISRI

Rais mteule wa Misri aanza kuunda serikali mpya.

Rais mteule wa Misri Mohamed Morsi
Rais mteule wa Misri Mohamed Morsi REUTERS/Egypt TV via REUTERS TV

Rais mteule wa Misri Mohamed Morsi ameanza kuunda serikali mpya hii leo wakati wafuasi wake wakiendelea kukaa katika eneo la Tahrir kuishinikiza serikali ya kijeshi inayoongoza kwa sasa kukabidhi madaraka kamili kwa kiongozi huyo wa chama cha Muslim Brothehood.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mpambano mkali ambao hatimaye umemruhusu Morsi kuyafikia makundi ya raia wanao unga mkono demokrasia, kiongozi huyo anatarajiwa kuwajumuisha mawaziri ambao watakuwa na msaada katika harakati zake.

Licha ya ushindi wa kihistoria alioupata Morsi siku ya Jumapili na kutangazwa kuwa rais wa kwanza aliyechaaguliwa na raia, bado analazimika kupambana na utawala wa kijeshi ambao unatafuta namna ya kuendelea kuwa na mamlaka makubwa huku uchumi ukiwa hatarini.

Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood ambacho kilimteua Morsi kuchukua nafasi ya rais aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak wamesema wataendelea kubaki katika viwanja vya Tahrir kushinikiza majenerali wa kijeshi wanaoongoza sasa kukabidhi madaraka kwa Morsi.