THAILAND

Wafuasi wa Red Shirts nchini Thailand wafanya maandamano makubwa.

Wafuasi wa Red Shirts katika maandamano.
Wafuasi wa Red Shirts katika maandamano. aljazeera.com

Maelfu ya raia nchini Thailand ambao ni wafuasi wa Red Shirts wamefanya maandamano makubwa mjini Bankok kufanya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kuangushwa kwa utawala wa kiimla na kuingia kwa utawala wa kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi hao ambao wanamuunga mkono waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo anaye ishi uhamishoni Thaksini Shinawatra walivalia mavazi mekundu na kukusanyika mjini Bankok kuwakumbuka wenzao ambao walipoteza maisha kutokana na harakati hizo za mapinduzi ya demokrasia .

Nchi hiyo imeshuhudia majaribio zaidi ya 20 ya mapinduzi nchini humo toka mwaka 1932 ambapo tangu kipindi hicho nchi hiyo imekuwa kwenye hali tete ya kisiasa hasa mara baada ya kuangushwa kwa serikali wa waziri mkuu Shinawatra na wanajeshi mwaka 2006.