SYRIA-UTURUKI

Wanachama wa NATO kukutana kujadili madai ya Uturuki dhidi ya Syria.

Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu RFI

Nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO zinatarajia kukutana kujadili madai yaliyotolewa na mwanachama wao Uturuki dhidi ya Syria kutungua ndege yake ya kivita iliyokuwa kwenye anga la kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umepangwa kufanyika baada ya waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu kunukuliwa akisema kuwa ndege yao ya kijeshi ilikuwa katika anga ya kimataifa na si anga la Syria kama ambavyo ilidaiwa awali.

Waziri mkuu wa Uturuki amekanusha vikali madai kuwa ndege hiyo ilikuwa katika anga la Syria kwa ajili ya uchunguzi na kusema kuwa iliingia kwa bahati mbaya kwa kuwa imekuwa mazoea wakati mwingine kwa ndege hizo kuingia kwenye anga hilo bila kufahamu.

Mkutano huo unatarajia kufanyika siku ya Jumanne ambapo mambo yatakayo jadiliwa ni pamoja na hatua zitakazo chukuliwa dhidi ya serikali ya rais Bashar Al assad ambayo inatajwa kuhusika kutungua ndege hiyo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Syria tayari ilishaonywa kabla ya kutekeleza shambulizi la kudungua ndege hiyo lakini ikakaidi na hivyo kuishambulia ndege hiyo ambayo ilikuwa kwenye mafunzo ya kawaida ya kijeshi.