SYRIA-UTURUKI

Wanajeshi zaidi wa Syria wakimbilia Uturuki.

Baadhi ya waasi wa jeshi la serikali ya Syria
Baadhi ya waasi wa jeshi la serikali ya Syria ctv.ca

Wanajeshi kadhaa wa jeshi la serikali ya Syria ikiwa ni pamoja na jenerali wa jeshi hilo wamekimbilia Uturuki usiku wa kuamkia leo na kujiunga na safu waasi walioweka kambi karibu na mpaka , huku mvutano ukizidi kuenea kati ya majirani hao wawili.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali mmoja, makanali wawili na askari 30 wakiongozana na familia zao wamevuka mpaka na kuingia Uturuki jana Jumapili,nakufanya idadi ya watu waliokimbilia Uturuki kufikia 196 shirika la habari la Anatolia limearifu.

Hatua hii inatimiza idadi ya majenerali 13 wanaotafuta hifadhi nchini Uturuki tangu uasi dhidi yautawala wa rais wa Syria Bashar al-Assad ulipoanza miezi 16 iliyopita.

Aidha raia 28 wa Syria wengi wao wakiwa wanawake na watoto pia wamekimbilia Uturuki na kupelekwa kwenye kambi ya wakimbizi katika jimbo la Sanliurfa karibu na mpaka.