UHISPANIA

Waziri mkuu wa Uhispania ataka ushirikiano katika ukanda wa ulaya.

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy REUTERS/Edgard Garrido

Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amewashinikiza viongozi wa Ulaya kuweka ratiba ya ushirikiano wa karibu wa ukanda wa sarafu ya Euro na kuzuia madhara yasiyotabirika katika uchumi wa dunia.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika siku ambayo serikali yake imetoa ombi rasmi la mkopo kwa wanachama wa ukanda wa ulaya ili kuinusuru nchi yake hasa taasisi za kibenki ambazo ziko hatarini, Rajoy ametoa wito kwa viongozi wa Ulaya wanaokutana kwa siku mbili kunzia siku ya Alhamisi kutilia maanani suala la kuiokoa sarafu ya Euro.

Aidha amesema kuwa Umoja wa Ulaya ni lazima uimarishe taasisi zake za kawaida za miundombinu ili wawekezaji waweze kurejesha imani katika sarafu moja kama sarafu imara, yenye kuaminika,

Waziri mkuu huyo pia amebadili ahadi yake ya kuchukua hatua mpya kwa ajili ya uchumi wa Uhispania uliofungwa ,ambapo ilipata kiwango cha ukosefu wa ajira kwa asilimia 24.4 katika robo ya kwanza ya mwaka huu.