JAPAN

Bunge Japan lapitisha muswada wa nyongeza ya ushuru wa biashara

Waziri mkuu wa Japan Yoshihiko Noda
Waziri mkuu wa Japan Yoshihiko Noda REUTERS/Kim Kyung-Hoon

Bunge nchini Japan limepitisha mswada wa kuongeza mara mbili ushuru wa kibiashara nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mswada huo wa utata umekuwa ukiungwa mkono na Waziri Mkuu Yoshinika Noda,ambaye anasema utasaidia kuinua uchumi wa taifa hilo.

Licha ya mswada huo kupitishwa, wabunge 57 wa chama tawala cha Waziri Mkuu Noda hawakupigia kura mswada huo unawaongezea kiwango cha maisha kwa wananchi wa Japan.

Ichiro Ozawa mmoja wa viongozi wa chama tawala amesema hueda akaunda chama kingine,suala ambalo ikiwa litafanyika,waziri Mkuu Noda atalazimika kuitisha uchaguzi mpya kwani inaaminika kuwa Ozawa atapata uungwaji mkubwa.

Hata hivyo wachambuzi wa maswala ya kisiasa nchini humo wanasema kuwa huenda wabunge wote wasimfuate Ichiro Ozawa ikiwa ataunda chama kipya jambo ambalo pia wanaeleza kuwa huenda likamfaya mwanasiasa huyo kuchukua muda kabla ya kuchukua uamuzi huo.