MISRI

Raisi Morsi ataka umoja kudumishwa nchini Misri

Raisi mpya wa Misri Mohammed Morsi,ataka umoja kudumishwa baina ya raia nchini humo.
Raisi mpya wa Misri Mohammed Morsi,ataka umoja kudumishwa baina ya raia nchini humo. REUTERS/Egypt TV via REUTERS TV

Rais Mteule wa Misri Mohamed Morsi ametoa wito wa kuwepo kwa umoja baina ya wananchi wa taifa hilo ili kuondokana na mgawanyiko ambao umeanza kujitokeza kipindi hiki ambacho anaanza mchakato wa kuunda serikali yake.

Matangazo ya kibiashara

Raisi Morsi amekutana na Uongozi wa Kijeshi uliokuwa unaongoza nchi hiyo tangu kufanyika kwa mapinduzi ya kuuangusha utawala wa Rais Hosni Mubarak ambapo amesema ataendelea kushirikiana nao.

Rais Morsi anatarajiwa kumtangaza Waziri Mkuu wake baadaye jumanne ili kuupa nafasi mchakato wa kuunda serikali kamili.

Hata hivyo Mkuu wa Sera za Kimataifa wa Umoja wa Ulaya EU Catherine Ashton ametoa wito kwa baraza la kijeshi la nchini Misri kuiheshimu serikali mpya ya kiraia.