RWANDA-DR CONGO

Serikali ya Rwanda yakanusha kuwafadhili waasi mashariki mwa Congo DR

Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Louise Mushikiwabo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Louise Mushikiwabo AFP

Serikali ya Rwanda imeendelea kukanusha vikali wao kushiriki kuwafadhili waasi wanaopambana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR wanaoendeleza mapambano mashariki mwa Congo DR.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema hayo akiwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa UN na kusema uzushi na taarifa ambazo zinaihusisha nchi hiyo kufadhili waasi wa DRC hazina ukweli wowote.

Mushikiwabo amesema serikali yake ipatiwe ushahidi unaodhihirisha wao ndiyo vinara wa kuwafadhili na kuwahifadhi waasi wanaopambana na serikaliya Kinshasa kutoka eneo la Mashariki.

Mapambano ya mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya demokrasia ya Congo dhidi ya waasi yamechangia adha nyingi kwa wakazi wa maeneo hayo ikiwemo vifo,watu kuyakimbia makazi yao,kukosekana kwa utulivu na hivyo watu kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji.