Brussels-EU

Umoja wa ulaya EU wazindua ruwaza yake

Kamishina wa Umoja wa Ulaya EU,Jose Manuel Barroso
Kamishina wa Umoja wa Ulaya EU,Jose Manuel Barroso telegraph.co.uk

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamezindua ruwaza yao inayowapa mamlaka zaidi kuhusu maswala ya umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mambo muhimu yalizinduliwa katika ruwaza hiyo ni pamoja na uundwaji wa ofisi itakayoshughulikia fedha za mataifa ya umoja huo.

Ofisi hiyo itakuwa na jukumu la kuthathmini na kushauri bajeti za mataifa ya umoja huo ili kusaidia kuepuka mgogoro wa uchumi katika mataifa.

Kamishena wa Umoja huo Jose Manuel Barroso amasema mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha zaidi umoja huo na kufungua milango ya mataifa hayo kuungana kisiasa,mapendekezo yanayotarajiwa kujadiliwa na wajumbe wa umoja huo siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii.

Umoja huo umekuwa ukikumbwa na changamoto ya kushughulikia uchumi wa mataifa ya umoja huo hasa Ugiriki na pia kwa sasa linashughulikia hali ngumu ya kiuchumi nchini Uhispania na Cyprus mataifa ambayo yameomba mkopo wa kifedha kutoka kwa Umoja huo.