SYRIA-UTURUKI

Uturuki yalalama UN juu ya vitisho vya Syria

Raisi Bashar Al Assad,wa Syria ambaye utawala wake unapingwa vikali na raia nchini humo
Raisi Bashar Al Assad,wa Syria ambaye utawala wake unapingwa vikali na raia nchini humo AFP

Uturuki imewasilisha rasmi malalamiko yake mbele ya Umoja wa Mataifa UN ikidai kutunguliwa kwa ndege yake kulikofanywa na Syria ni kitisho juu ya amani katika eneo hilo na lazima juhudi zifanyike kudhibiti vitendo kama hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Malalamiko hayo ya Uturuki yanawasilishwa kipindi hiki ambacho Wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO wanakutana jumanne kujadili hatua ya kutunguliwa kwa ndege hiyo.

Tayari Umoja wa Ulaya EU kupitia Mkuu wake wa Sera za Kimataifa Catherine Ashton wamelaani shambulizi hilo na tayari wametangaza kuongeza vikwazo kwa nchi ya Syria.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amesema wakati umefika kwa Baraza la Usalama la kufanya kila linalowezekana ili kuwalinda wananchi.

Syria imeendelea kukabiliwa na shinikizo linalomtaka Rais Bashar Al Assad kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo kuruhusu demokrasia kuchukua mkondo wake au akae kando.