DRC

UN yajipanga upya nchini DRC, kundi la Konny kushughulikiwa

RFI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapitia upya mamlaka ya Vikosi vyake vinavyoshika doria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC baada ya siku za hivi karibu kuzuka malalamiko ya wao kutofanyakazi zao ipasavyo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja wakati Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini ikiendelea kushuhudia maspigano makali na kuchangia kutetereka kwa hali ya usalama katike eneo hilo na kuzua maswali kazi za MONUSCO kama zinafanyika ipasavyo.

Viongozi kadhaa wa Vyama na Mashirika ya Kiraia wameelekea nchini Marekani kwenye makao makuu ya Baraza la Usalama kudai mageuzi ya mamlaka ya vikso hivyo vya Umoja wa mataifa kama anavyoeleza Robert Mabala.

Wakati huohuo Wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa UN na Umoja wa Afrika AU wamesema kuwa wanaendelea kusaka mbinu kabambe katika kuhakikisha wanalimaliza Kundi la Waasi la LRA linaloongozwa na Joseph Kony.

Kundi la Waasi la LRA limeendelea kuwa hatari kwa usalama wa raia katika nchi za Uganda, Jamhuri ya Congo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na kuajiri watoto wadogo kwenye jeshi lao.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu katika Eneo la Afrika ya Kati UNOCA Abou Moussa amesema watafanya kila linalowezekana katika kulimaliza kundi la LRA.