RWANDA-DRC-UN

Rwanda yalaani ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu waasi nchini DRC

AFP PHOTO / JUNIOR D.KANNAH

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amelaani na kukashifu ripoti ya Umoja wa mataifa UN iliyoitaja serikali ya Kigali kuhusika na kuwafadhili waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo DRC wanaopigana na serikali.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema kuwa nchi yake inatarajia kuwasilisha ushahidi wake kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa kukanusha madai ya nchi yao kufadhili waasi.

Pia waziri huyo ameahidi kutoa ushahidi kuonesha jinsi gani Umoja wa mataifa unapaswa kulaumiwa kutokana na machafuko yanyoendelea nchini DRC.

Waziri Mushikiwabo amesema kuwa ripoti iliyotolewa na UN inaegemea upande mmoja na ndani yake hakuna utafiti wa kina uliofanywa wakati wa kuandaa ripoti hiyo inayolenga kuharibu picha ya Rwanda.

Amesema kuwa ushahidi watakaotoa utaonyesha ukweli na kufuta picha mbaya inayojaribu kuonyeshwa na Umoja wa Mataifa Rwanda imekuwa ikiwasaidia waasi wa M23 wa DRC.