JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

Hukumu ya Raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC Thomas Lubanga kutolewa Julai 10

REUTERS/Michael Kooren

Hukumu ya Raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC Thomas Lubanga aliyekutwa na hatia ya kutumia watoto katika vita na vitendo ngono inatarajiwa kutolewa mwezi ujao.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC yenye makao yake The Hague nchini Uholanzi imesema leo itatoa hukumu hiyo Julai 10, mwaka huu hukumu inayokuja kutokana na hatia hiyo.

Tomas Lubanga mwenye umri wa miaka 51 alikutwa na hatia mwezi Mach mwaka huu ya kushirikisha watoto katika kundi la lake la kijeshi la waasi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia mwaka 2002 mpaka mwaka 2003.

Hukumu hiyo itakua ya kwanza kutolewa na mahakama ya ICC ambayo imekuwa ikishughulikia kesi hiyo kwa kipindi cha miaka kumi sasa na hati ya hukumu yake itasomwa wazi kuanzia majira ya saa 4.30 asubuhi julai 10.

Tomas Lubanga alikutwa na hatia ya kuwateka watoto wenye umri wa kuanzia miaka kumi na moja na aliwalazimisha kupigana katika vita katika mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC MKOA ambao una utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu.

Wakati kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo namna watoto wa kike walivyotumiwa kama watumwa na kufanyishwa mapenzi wakati watoto wa kiume walipatiwa mafunzo ya kupigana vita.

Mwendesha mashitaka mkuu wa wa zamani wa ICC, Luis Moreno-Ocampo mapema mwezi huu kabla ya kumaliza mkataba wake aliiomba mahakama hiyo imfunge miaka 30 jela kwa sababu kesi yake iangusa hisia za jumuiya ya kimataifa.