Vikundi vya upinzani nchini Syria vyakataa pendekezo la Koffi Annan

REUTERS/Denis Balibouse

Rais wa Syria Bashar Al Assad ameseme mgogoro unaoendelea katika nchi hiyo utapata ufumbuzi kutoka kwa wananchi wa taifa hilo huku akisisitiza mpango wa mapendekezo sita ya Mpatanishi Kofi Annan unastahili kutekelezwa.

Matangazo ya kibiashara

Kauli yake inakuja siku moja baada ya Annan kutoa pendekezo la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ikijumuisha pande zinazokinzana ili kuweza kumaliza umwagaji wa damu uliodumu kwa zaidi ya miezi kumi na sita sasa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amesema pendekezo hilo la Annan ambalo ataliwakilisha kwenye mkutano na Mawaziri wa Mambo ya nje wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama utakuwa na mafanikio.

Hata hivyo vikundi vingi vya upinzani nchini Syria vimesema kuwa havitakubali mapendekezo ya Koffi Annan kama serikali ya mpito itamjumuisha rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad.

Vikundi hivyo vinavyopingana na serikali ya Assad vimesema vitakuwa tayari kuunda serikali ya mpito kama rais huyo ataondoka madarakani na vinginevyo hawako tayari kufanya hivyo.

Bwana Koffi Annan anatarajiwa kuwasilisha maprndekezo hayo mapya ya kuzitaka pande zinazokinzana kuunda serikali ya mpito katika mkutano wa Umoja wa Mataifa jumamosi wiki hii.