MALI

Waasi wa kiislamu nchini Mali watishia taifa litakalojiunga katika jeshi la pamoja

Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine,nchini Mali
Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine,nchini Mali Reuters/Adama Diarra

Makundi ya waasi wa kiislamu nchini Mali yametishia kwa nchi yoyote itakayojiunga na jeshi la pamoja kwa ajili ya kuingilia mambo ya kijeshi nchini humo ikiwa ni baada ya jumuiya ya kiuchumi ya afrika magharibi ECOWAS kuunda jeshi la pamoja la kushughulikia amani nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

Makundi hayo ikiwemo Ansar Dine na Al-Qaeda huko Maghreb, yalianzisha sharia za kiislam kaskazini mwa Mali na kushuhudia zikishindwa kutekelezeka.

Nao wakuu wa jumuiya ya kiuchumi ya kanda ya Afrika magharibi ECOWAS walikutana nchini cote d' Ivoire kujadili namna ya kumaliza machafuko na kufikia uamuzi wa kutuma jeshi la watu elfu tatu na mia tatu.

Wakati huohuo kwa upande wa kundi la kiislamu la MUJAO, limedai kuhusika na shambulizi la ijumaa huko Algeria ambapo walishambulia makao makuu ya polisi nchini humo na kuua mtu mmoja na watatu kujeruhiwa.