SUDAN-SUDAN KUSINI

Maadhimisho ya Mwaka mmoja wa uhuru wa Sudan Kusini, yakubaliana na Sudan kukomesha vitendo vya kinyama

Raisi wa Sudan Omar Al Bashir
Raisi wa Sudan Omar Al Bashir AFP

Sudan na Sudan ya kusini zimekubaliana kukomesha vitendo vya kinyama katika eneo la mafuta huko mpakani kwa kuingia makubaliano ya maandishi.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yanakuja baada ya mazungumzo ya mwisho ya huko Ethiopia yakifuatiwa na maadhimisho ya sherehe za mwaka mmoja hii leo tangu uhuru wa sudan ya kusini.

Waziri wa ulinzi wa Sudan Abdelrahim Mohamed amesema kuwa makubaliano ya pande hizo mbili yamelenga kusitisha mapigano na kumaliza tofauti zao ambapo mazungumzo zaidi yanatarajiwa kuendelea hapo Julai 11 baada ya maadhimisho ya uhuru.