JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Amani mashariki mwa Congo kujadiliwa leo katika mkutano wa nchi za maziwa makuu

Viongozi wa nchi za maziwa makuu wakiwa katika picha ya pamoja
Viongozi wa nchi za maziwa makuu wakiwa katika picha ya pamoja fullshangweblog.com

Viongozi wa kanda ya Maziwa Makuu watakutana leo mjini Adis Ababa Ethiopia kujadili vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afisa mwandamizi wa Umoja wa Afrika amearifu. 

Matangazo ya kibiashara

Kamishna wa Amani na Usalama Ramtane Lamamra hakubainisha idadi ya viongozi watakao hudhuria, hata hivyo vyanzo vimeliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa rais wa DR Congo Joseph Kabila na Rais wa Rwanda Paul Kagame wanatarajiwa kuwepo katika mkutano huo.

Iwapo marais hao wawili watakutana uso kwa uso, itakuwa mara yao ya kwanza tangu maofisa wa juu wa Rwanda kushutumiwa na Umoja wa Mataifa kuunga mkono kundi la waasi wa kitutsi la M23, ambao wamekuwa wakipambana na askari wa jeshi la serikali ya DR Congo mashariki mwa nchi hiyo tangu mwezi Aprili shutuma mabazo Rwanda imekuwa ikizikanusha.