Korea Kaskazini

Kim Jong-Un atangazwa kuwa Jemedari Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ametangazwa kuwa Jemedari wa Taifa hilo la Kikomunisti hatua inayokuja siku mbili baada ya kufanyika mabadiliko ya nafasi ya Mkuu wa Jeshi.

Matangazo ya kibiashara

Nafasi hiyo  ya Jemedari ilikuwa inashikiliwa na Baba yake Jong-Un ambaye alikuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini Marehemu Kim Jong-Il, ambaye alifariki kutokana na kukabiliwa na maradhi ndicho cheo cha juu sana zaidi nchini humo.

Televisheni ya taifa nchini Korea Kaskazini ndiyo ambayo imetangaza hatua hiyo ya Jong-un kuwa Jemedari wa kitu ambacho wamesema kimefanywa ili kumuongezea madaraka na uwezo wa kuongoza.

Wachambuzi wa Masuala ya Usalama na kisiasa nchini Korea Kaskazini wamesema hatua hiyo imedhihirisha uaminifu na hata ukomavu wa Kiutawala ambao anao kwa sasa Jong-Un.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini Jong-Un alikuwa Jenerali mnamo mwezi Septemba mwaka elfu mbili na kumi ikiwa ni sehemu ya kumweka karibu kujua masuala ya utawala wa kijeshi.

Kim Jong-Un amepewa cheo hicho siku mbili  baada ya kiongozi wa majeshi Ri Yong-ho kuondolewa  kwa sababu ya maradhi.