SYRIA

Vikosi vya serikali nchini Syria vyashambulia kambi ya wapinzani mjini Damascus.

Vikosi vya serikali  vyashambulia mji wa Damascus
Vikosi vya serikali vyashambulia mji wa Damascus skynews.com.au

Vikosi vya serikali ya Syria vimefanya shambulio nje ya ngome ya upinzani huko Damascus, baada ya waasi kuteka eneo la njia panda ya mipaka ya Iraq na Uturuki huku kukiwa na ongezeko kubwa la idadi ya vifo. 

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji waasi pia walipambana na askari katika vitongoji kadhaa ya Aleppo siku ya Ijumaa katika kile ambacho waangalizi wa haki za binadamu nchini humo wanadai kuwa ni mapigano makali kuwahi kutokea katika mji huo.

Katika Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama lilipiga kura kwa kauli moja kutoa kauli ya mwisho ya kuongeza siku 30 kwa waangalizi ambao wanawajibika kusimamia mpango wa amani nchini Syria, kazi ambayo hata hivyo ilisitishwa mnamo Juni 16 kutokana na kuendelea kwa machafuko.