EU-SYRIA

Umoja wa Ulaya wazidi kuibana Syria kuhusu mgogoro

REUTERS/Kimmo Mantyla/Lehtikuva

Umoja wa Ulaya, EU umekubaliana kuweka vikwazo kwa utawala wa Rais wa Syria, Bashar Al Assad kama shinikizo la kumaliza mgogoro unaoendelea nchini humo na kusababisha mauaji ya raia.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa EU wamekubaliana kuwa nchi wanachama watakuwa wakikagua meli na ndege zote ambazo zitakuwa zinahisiwa kubeba mizigo inayotumiwa na watu wa Syria ili kudhibiti vifaa ambavyo vinaweza kuvuruga amani nchini humo.

Wamesema kuwa nchi wanachama endapo watahisi meli au ndege katika mipaka ambayo inasadikiwa kuwa ni ya Syria zitalazimika kutuma wachunguzi wa kukagua vyombo hivyo vya usafiri.

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa 27 wameanza mazungumzo na kukubaliana kuzuiwa kwa mali za watu 26 wa Syria na mashirika matatu ambayo yako karibu na utawala wa Bashar Al Assad.

Hatua hizo zinachukuliwa ili kuubana zaidi utawala wa Syria ili kukomesha machafuko yanayondelea kusababisha vifo vya raia wasio na hatia nchini humo ambapo mpaka sasa watu wapatao 19,000 wamepoteza maisha.