SYRIA

Wapinzani wa Syria watakiwa kujiandaa kuchukua madaraka

REUTERS

Jenerali wa jeshi la Syria aliyeasi Manaf Tlass ametoa wito kwa wananchi wa Syria kuungana wakati huu ambapo jeshi huru la Syria limeanza kufanikiwa kutwaa baadhi ya maeneo muhimu.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo inatolewa wakati ambapo kumeripotiwa mapigano makali kwenye mji wa Allepo na Damascus ambapo wanajeshi wa serikali wameendelea na operesheni ya kujaribu kurejesha maeneo yaliyotekwa na waasi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton ameendelea kusisitiza nchi yake kuwaunga mkono waasi na kuongeza kuwa kinachoshuhudiwa sasa kwenye upande wa waasi ni wazi kuwa utawala wa Asad umefikia kikomo.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa iawapo nchi ya Syria itatumia silaha za maangamizi hali itazidi kuwa mbaya zaidi nchini humo.

Juma hili serikali ya Syria kupitia msemaji wake ilikiri kumiliki silaha za maangamizi na kuahidi kuzitumia kwa taifa lolote litakalojaribu kuivamia kijeshi lakini sio kwa wananchi wake.