Serikali ya Ugiriki yajipanga kupata mkopo wa dola bilioni 11.6

REUTERS/Yves Herman

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya EU Jose Manuel Barroso yupo nchini Ugiriki akiendelea na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Taifa hilo Antonis Samaras ikiwa ni sehemu ya kuangalia hatua ambazo zimepigwa na serikali ya Athens inayosaka mkopo.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ugiriki inaendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inapatiwa mkopo wa dola bilioni kumi na moja nukta sita na tayari imeenza kutekeleza mashariki ya Umoja wa Ulaya EU na Shirika la Fedha Duniani IMF la kubana matumizi.

Barroso anakutana na Waziri Mkuu Samaras ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu inayokuja kwa lengo la kuonkoa uchumi uliyoyumba wa nchi ya Ugiriki inayojipanga upya.

Waziri wa Fedha wa Ugiriki Yannis Stournaras amesema wasingependa ombi lao lisogezwe mbele badala yake wangepata mkopo huo ili kuanza mchakato wa kujenga upya uchumi wa taifa hilo.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Fedha Duniani IMF Poul Thomsen amesema mazungumzo yao na viongozi wa serikali yamekwenda vyema na wanaimani kila kitu kitaafikiwa na Athens itapata mkopo huo.