Kenya-Venezuela

Kaimu balozi wa Venezuela nchini Kenya Olga Fonseca anyongwa hadi kufa

Aliyekuwa kaimu balozi wa Venezuela nchini Kenya,Olga Fonseca Gimenez
Aliyekuwa kaimu balozi wa Venezuela nchini Kenya,Olga Fonseca Gimenez ovario.wordpress.com

Kaimu balozi wa Venezuela nchini kenya Olga Fonseca Gimenez amekutwa na mauti baada ya kunyongwa na mwili wake kukutwa nyumbani kwake jijini Nairobi.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la polisi nchini kenya kupitia mkuu wa polisi Anthony Kibuchi amethibitisha kifo cha kaimu balozi huyo na kuongeza kuwa mwili wa balozi Olga bado upo eneo la tukio ili kuwezesha uchunguzi wa awali katika kubaini chanzo cha kifo chake.

Kibuchi amesema kuwa wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Venezuela nchini Kenya wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi kufuatia kifo hicho cha kaimu balozi Olga Fonseca Gimenez.

Kufuatia tukio hilo tayari nchi ya Venezuela kupitia wizara ya mambo ya nchi za nje imeelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho na kuongeza kuwa ina imani na mamlaka ya Kenya juu ya kuchunguza na kubainisha wahusika wa kifo hicho huku ikiahidi kutoa msaada wa namna yoyote utakaohitajika.

Balozi Fonseca alichaguliwa kukaimu wadhifa huo mnamo mwezi June tarehe 25 mwaka huu.