CHINA

Polisi China wapambana na waandamanaji wanaopinga uchafuzi wa mazingira

submitlist.info

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda cha makaratasi huko mashariki mwa China wamepambana na polisi mapema jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la ufaransa AFP ,Waandamanaji hao wamepindua magari mawili na kuvamia ofisi ndogo za serikali katika pwani ya Qidong jirani na Shanghai.

Maelfu ya raia wamekusanyika nje ya ofisi ndogo za serikali huku wakilaani baadhi ya vitendo vya ulaji rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watendaji katika mamlaka na kuchangia kutofanikiwa kwa juhudi za kupinga uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda cha karatasi mjini humo.

Kufuatia kuongezeka kwa viwanda nchini china kumechangia kuongezeka kwa mgogoro na maandamano dhidi ya uharibifu wa mazingira nchini humo.