India

Takriban watu milioni mia tatu wakosa umeme nchini India

Habiria wa Treni wakisubiri usafiri baada ya umeme kukatika
Habiria wa Treni wakisubiri usafiri baada ya umeme kukatika

Eneo la kaskazini mashariki mwa India limekumbwa na tatizo kubwa la kukatika kwa umeme Jumanne hii Julay 31, masaa 24, ikiwa ndio tukio kubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 10 iliopita lililo sababisha watu milioni mia tatu kukosa umeme, lakini tukio la sasa limepelekea watu milioni sita kukosa umeme.

Matangazo ya kibiashara

Eneo zima la kaskazini na mashariki mwa India, kuanzia Rajasthan hadi
Calcutta au Bengale na kupitia New Delhi umeme umekatika ghafla mchama wa jumanne. Treni mia saba zimesimama, mitaa ya barabarani yamezimika katika miji mingi kufuatia tukio hili na hivo kusababisha msongamano mkubwa wa watu na magari. Wachimba migodi wanasadikiwa kuzuiliwa kufuatia jinamizi hilo.

Wizara ya nishati imetangaza kuendesha shughuli za dharula katika hospitali mbalimbali na uwanja wa ndege kabla ya siku hii kumalizika hali ambayo haijulikana itadumu kwa muda gani.

Jimbo la Uttar Pradesh lenye wakaazi milioni mia mbili kaskazini mwa India linatuhumiwa kuwa chanzo cha tukio hilo baada ya kuongeza idadi ya matumizi ya umeme yaliosababisha umeme kukatika. Wizara ya Nishati imetangaza kuunda tume itayoendesha uchunguzi kujuwa chanzo cha kukatika kwa umeme.