Syria

Wapiganaji wa upinzani nchini Syria wafaanikiwa kuteka kituo muhimu katika mji wa Allepo

Kifaru cha kijeshi kilicho shambuliwa kwa roketi jumatatu Julay 30 katika mji wa Allepo
Kifaru cha kijeshi kilicho shambuliwa kwa roketi jumatatu Julay 30 katika mji wa Allepo RFI/Jérôme Bastion

Mapigano yameingia siku ya nne mfululizo katika mji wa Allepo nchini Syria kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani. Wapiganaji wa upinzani wamefaanikiwa kuteka kituo muhimu katika mji huo wa pili wa Syria, ambapo sasa watapata urahisi wa kusafirisha silaha na vifaa vyao muhimu vya kivita.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Syria laendelea kupambana katika kila kona ya mji na majumba ya Aleppo. Waandishi wa habari waliokatika kila upande wamethibitisha kuendelea kwa mapigano makali kati ya jeshi la Syria na waasi wa jeshi huru la Syria.

Wanajeshi wa Syria wametangaza kufaanikiwa kuurejesha kwenye himaya yao kata ya Salah Eddine na njiapanda muhimu ya Jendoli, habari ambayo imekanushwa na waasi ambao wamethibitisha kuwearejesha nyuma wanajeshi wa serikali.

Duru sahihi zimethibitisha kuwa jeshi la serikali ya Syria limefaanikiwa kusonga mbele kwqenye uwanja wa mapambano, licha ya kuwepo bado waasi katika vitongoji mbalimbali vya mji huo, ambapo haijulikani iwapo wanajeshi wa serikali wataendelea kujigamba kupata ushindi au la.

Mbinu ya wanajeshi wa serikali ya Syria ni kuhakikisha wamewazingira waasi na baadae kuwashambulia hatua kwa hatua, licha ya kwamba mbinu hiyo inachukuwa muda mrefu.

Maelfu ya watu wanakimbilia nchini Uturuki na Iraq kutafuta hifadhi kutokana na mapigano hayo ambayo pia yamewaacha watu wengi majeruhi.

Katika hatua nyingine, Uturuki na Marekani wameendelea na mazungumzo ya namna ya kumaliza mzozo huo na pamoja na maswala nyeti wanayojadili ni pamoja na namna rasi Bashar Al Assad atakavyoondolewa mamlakani.

Rais Barrack Obama na waziri Mkuu wa Uturuki wamekuwa wakizungumza kwa njia ya simu kuhusu hatima ya syria.